HabariPilipili FmPilipili FM News

Moto Waangamiza Watoto Wawili Kwale.

Watoto wawili wamefariki baada ya nyumba walimokuwa wamelala ndani kuteketea katika eneo la Kona ya Musa kaunti ya Kwale jana usiku.

Miili ya watoto hao imeteketea kiasi cha kutotambulika katika mkasa huo wa moto ulioanza mwendo wa saa mbili jana usiku, ambao unadaiwa kusababishwa na hitilafu ya nguvu za umeme.

Inadaiwa kuwa watoto hao walikuwa wamelala pekee yao kwani wazazi wao walikuwa hawajarudi nyumbani kutoka kazini.

Wazima moto walichukuwa takriban masaa matatu kuuzima moto huo.

Miili ya watoto hao imepelekw akatika hifadhi ya maiti katika hospitali ya rufaa Msambweni huku polisi wakianzisha uchunguzi

Show More

Related Articles