HabariMilele FmSwahili

Mtu 1 afariki kutokana na mafuriko Taveta

Mtu mmoja amethibitishwa kufariki huku zaidi ya familia 20 katika kijiji cha wanganga eneo la Taveta zikiathiriwa na mafuriko kufuatia mvua inayoendelea kunyesha sehemu hiyo. Mmoja wa viongozi wa kijiji hicho Agostine Juma amesema familia hizo zimekosa makao huku kina mama na watoto wakiathirika zaidi. Familia hizo sasa zinategemea misaada kutoka kwa wahisani ili kukabiliana na janga hili.

Show More

Related Articles