HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosTop StoriesVideos

Mahakama yabatilisha uchaguzi wake kama Mbunge wa Embakasi East

Mahakama kuu hapa Nairobi imefutilia mbali ushidi wa mbunge wa Embakasi Mashariki Paul Ongili maarufu kama Babu Owino, kutokana na kile mahakama imetaja kama dosari zilizokumba uchaguzi huo.

Mahakama pia imefutilia mbali ushindi wa Joyce Emanikor kama mwakilishi wa kina mama wa kaunti ya Turkana.

Haya yalijiri huku mahakama kuu ikishikilia ushindi wa James Gakuya mbunge wa Embakasi Kaskazini na Mishi Mboko mbunge wa Likoni na wengineo, akiwemo Moses Lessonet wa Eldama Ravine.

Kufikia sasa, ushindi wa waheshimiwa 11 wakiwemo magavana 3 umefutiliwa mbali.

Show More

Related Articles