HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosTop StoriesVideos

Afisa Mkuu Lily Koros apewa likizo ya lazima na Waziri wa Afya

Afisa mkuu mtendaji wa Hospitali kuu ya Kenyatta  Lily Koros amepewa likizo ya lazima na Waziri wa Afya Sicily Kariuki.
Haya yanajiri baada ya hospitali ya Kenyatta kwa mara nyingine kujipata katika njia panda baada ya daktari wa kitengo cha upasuaji kumfanyia mgonjwa asiyefaa upasuaji wa ubongo.
Aidha waziri Kariuki ameomba msamaha kwa wakenya  huku akiahidi kuwa gharama ya matibabu ya wagonjwa hao wawili waliojipata kwenye masaibu hayo itasimamiwa kikamilifu na NHIF.

Show More

Related Articles