HabariPilipili FmPilipili FM News

Marwa Akula Kiapo Cha Kuhudumu Kama Katibu Katika Wizara Ya Ugatuzi.

Shughuli ya kuwalisha kiapo makatibu  wapya na manaibu wao inaendelea katika ikulu ya rais jijini Nairobi.

Nelson Marwa aliyekuwa mshirikishi wa serikali kuu kanda ya pwani na ambaye sasa atahudumu kama katibu katika wizara ya ugatuzi nchini,pamoja na Proffessa Hamadi Iddi Boga atakaye hudumu kama katibu katika wizara ya kilimo ni miongoni mwa makatibu waliolishwa kiapo hivi leo.

 

Wengine ni Kamau Thuge aliyeteuliwa katibu katika wizara ya fedha nchini, Joseph Njoroge kawi, Julius Muia katibu katika wizara ya mipango miongoni mwa wengine.

Rais Uhuru Kenyatta akiongea baada ya hafla ya kuwalisha kiapo kukamilika amewataka kuwajibikia majukumu yao ya kuwahudumia wananchi, akisema serikali iko tayari kufanya kazi nao.

 

 

 

 

 

Show More

Related Articles