HabariMilele FmSwahili

Upepo mkali wang’oa paa za madarasa 3 katika shule ya msingi ya Nzwii, Kibwezi

Wanafunzi zaidi ya 100 katika shule ya msingi ya Nzwii iliyoko Kambu huko Kibwezi kaunti ya Makueni hawana pa kusomea baada ya upepo mkali kungoa paa za madarasa matatu usiku wa kuamkia leo. Kwa mujibu wa mkuu wa elimu eneo la Kibwezi Kennedy Machora wanafunzi walioathirika ni wa darasa la tatu nne na tano. Ametoa wito wa wahisani kujitokeza kusaidia katika ukarabati wa madarasa hayo.

Show More

Related Articles