HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosVideos

Waziri wa Usalama atangaza vita dhidi ya pombe haramu

Waziri wa usalama wa taifa Fred Matiang’i amewaonya watengenezaji na wauzaji wa pombe haramu kwamba chuma chao ki motoni, huku serikali ikianzisha rasmi kampeni ya kukabiliana na vinywaji hivyo haramu pamoja na dawa za kulevya.
Katika mkutano uliohudhuriwa na wadau mbalimbali wakiwemo inspekta jenerali wa polisi Joseph Boinnet pamoja na maafisa wa mamlaka ya kupambana na dawa za kulevya, NACADA, mahakama imelaumiwa kwa kile kilichotajwa utatizaji wa haki.
Matiang’i vile vile ameamuru makamishna wa kaunti kuwapiga kalamu maafisa wa utawala wanaoshirikiana na watengenezaji pombe haramu.

Show More

Related Articles