HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosVideos

Mbunge wa Tiaty atetea mswada anaopendekeza kugeuza uongozi

Huenda gharama ya uchaguzi mkuu wa mwaka wa elfu mbili na ishirini na mbili ikapungua kwa asilimia ishirini na tano, iwapo bunge litapitisha mswada wa marekebisho unaopendekeza kuwepo kwa nafasi ya waziri mkuu kwenye katiba.
Kamati ya bajeti bungeni ambayo imekuwa ikitathmini mswada unaopendekezwa na mbunge wa Tiaty William Kamket imesema walipa ushuru wataokoa shilingi bilioni kumi na moja mswada huo ukipitishwa, kwani wapiga kura hawatamchagua rais, seneta na vile vile mwakilishi wa akina mama kama ilivyo kwa sasa.
Hata hivyo kama anavyotuarifu Kiama Kariuki,mswada huo una safari ndefu na yenye misukosuko kabla ya kufanywa sheria, kwani utakuwa unawakwaruza viongozi wengi ambao wanapima ubabe wao kupitia kura.

Show More

Related Articles