HabariPilipili FmPilipili FM News

Wafanyikazi Wa Nakumatta Nyali Waachishwa Kazi

Wafanyakazi wa duka la jumla la Nakumatt Nyali hapa Mombasa wanalalamikia kuachishwa kazi kinyume cha sheria bila kupewa ilani.

Wafanyikazi hao wanasema wanataka walipwe mishahara yao ya takriban miezi minane ili waweze kukidhi majukumu yao ya  kifamilia.

Aidha wameitaka serikali pamoja na katibu wa muungano wa wafanyikazi nchini COTU Francis Atwoli kuingilia kati suala hilo ili wapate haki yao.

 

Show More

Related Articles