HabariMilele FmSwahili

Makamishna wa tume ya huduma za bunge waapishwa

Makamishna wa tume ya kuangazia maslahi ya wabunge(PSC) wameapishwa rasmi. Spika wa bunge Justine Muturi aliye pia mwenyekiti wa tume hiyo alikua wa kwanza kula kiapo kabla ya kushuhudia kuapishwa kwa makamishna wengine. Walioapishwa ni maseneta George Khanir na Aaron Cheruiyot kisha wabunge Aden Keynan,Ben Momanyi,Naomi Shaban na Asiha Jumwa. Akiongea baada ya hafla hiyo,spika Muturi amewataka makamishena hao kuanza kazi mara moja na kuhakikisha wanawakilisha maslahi ya wabunge..

Show More

Related Articles