HabariMilele FmSwahili

Kina mama 8000 hufariki kila mwaka wanapojifungua nchini

Kina mama 8000 hufariki kila mwaka wanapojifungua nchini . Kulingana na ripoti ya utafiti uliofanywa katika miaka miwili iliyopita kuhusiana na vifo hivyo iliyofanywa na wizara ya afya asilimia 73 ya vifo vinatokana na kina mama hao kupuuzwa. Aidha ripoti hiyo imebaini kuwa zaidi ya asilimia 42 ya vifo hivyo hutokea katika hospitali za umma za Level 4. Uhaba wa vifaa pia umetajwa kuchangia vifo hivyo. Ripoti ya utafiti huo iliyotolewa na mkuu wa kitengo cha afya ya mama katika wizara ya afya. Dkt Gondi J.O pia imebaini kuwa kaunti 15 huripoti asilimia 90 ya visa hivyo. Mkurugenzi wa huduma za matibabu dkt Jackson Kioko amesema uchunguzi unaendelea katika vituo vya afya vya umma kwa lengo la kuwachukulia hatua wahudumu wa afya wanaochangia vifo hivi.

Show More

Related Articles