HabariMilele FmSwahili

Katibu Mkuu wa chama cha wanafunzi auawa kwa kupigiwa risasi Meru

Uchunguzi umeanzishwa huko Meru kufuatia kisa ambapo polisi wanadaiwa kumuua kwa kumpiga risasi Katibu mkuu wa muungano wa wanafunzi katika chuo cha Meru Evans Njoroge maarufu Kidero. Evans alikuwa akiongoza maandamano ya wanafunzi hao Jumanne kulalamikia kuongezwa karo ya chuo na usimamizi mbaya wa taasisi hiyo kabla ya makabiliano kuzuka baina ya polisi na wanafunzi. Inadaiwa kiongozi huyo aliandamwa na polisi waliomfuata hadi shamba moja liliko karibu na chuo ambapo walimpiga risasi, madai ambayo sasa yanachunguzwa.

Show More

Related Articles