HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosVideos

Ugavi wa chakula waanzishwa kaunti za Tana River na Kilifi

Siku moja tu baada ya serikali kutangaza ugavi wa chakula cha msaada katika kaunti nne zilizoathirika zaidi na baa la njaa, shughuli hiyo imeanza hii leo katika kaunti ya Tana River na ile ya Kilifi.
Hatua hiyo inawadia huku waziri wa mazingira Keriako Tobiko akizindua jopo la wanachama 17, litakalo andaa ripoti kuhusu hali ya misitu na maeneo ya chemi chemi kote nchini, kufuatia taarifa iliyopeperushwa na runinga ya K24 iliyoangazia uharibifu wa misitu wiki chache zilizopita.

Show More

Related Articles