HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosVideos

Katibu Mkuu wa chama cha wanafunzi auawa kwa kupigiwa risasi

Mwanafunzi mmoja wa chuo kikuu cha Meru ameuawa kwa kupigwa risasi katika maandamano shuleni humo.
Inadaiwa mwanafunzi huyo ambaye hadi kifo chake alikuwa katibu mkuu wa muungano wa wanafunzi katika chuo hicho alipigwa risasi na maafisa wa polisi.
Inasemekana Evans Njoroge, alipigwa risasi katika vuta nikuvute wakati polisi waliitwa kudhibiti usalama baada ya wanafunzi kushiriki maandamano kushinikiza kujiuzulu kwa naibu chansela wa chuo hicho na nyongeza ya karo.

Show More

Related Articles