HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosVideos

Mbunge Kassait Kamket atayarisha mswada wa kurekebisha katiba

Mbunge wa Tiaty Kassait Kamket sasa ameandika mswada anaopania kuwasilisha mbele ya bunge, ambao unapendekeza katiba kufanyiwa marekebisho ili kuunda nafasi ya waziri mkuu na kupunguza mamlaka ya rais.
Kwenye mswada huo ambao K24 imepata nakala yake, Kassait vile vile anapendekeza rais kuchaguliwa kwa muhula mmoja tu wa miaka saba , na wala sio mihula miwili ya miaka mitano kila muhula kama ilivyo kwa sasa.
Kama anavyoarifu Kiama Kariuki, iwapo mswada huo utapitishwa na kuwa sheria, hakutakuwepo tena na nafasi ya naibu wa rais kama anavyotuarifu Kiama Kariuki.

Show More

Related Articles