HabariMilele FmSwahili

Gavana wa Nairobi Mike sonko afanyia mabadiliko baraza lake la mawaziri

Gavana wa Nairobi Mike Mbuvi Sonko amefanyia mabadiliko baraza lake la mawaziri. Kwenye ilani aliyotia saini jana gavana Sonko amemteua Danvas Makori waziri mpya wa fedha huku aliyekuwa akihudumu kwenye wizara hiyo Veska Kangongo akiteuliwa waziri wa ugatuzi. Larry Wambua ambaye alikuwa waziri wa ugatuzi amechukuwa wadhifa wa waziri wa mazingira naye Emmah Mukuhi akichaguliwa waziri wa teknolojia na mawasiliano. Charles Kerich amechaguliwa waziri wa ardhi akitwaa mahala pa Peter Njuguna ambaye sasa ni waziri wa Kilimo. Hitan Hitan Majevdia anasalia kuwa waziri wa afya Allan Igambi waziri wa Utalii na Janet Ouko waziri wa elimu.

Show More

Related Articles