HabariMilele FmSwahili

Kesi ya kupinga ushindi wa Aden Duale yatupiliwa mbali

Mahakama kuu imetupiolia mbali kesi ya kupinga ushindi wa mbunge wa Garisa mjini Aden Duale. Jaji Hedwig Ongudi ameamua kuwa mlalamishi aliyekuwa naibu spika Farah Maalim amefeli kudhibitisha madai kuwa baadhi ya wapiga kura walihongwa au kuzuiwa kupiga kura. Jaji Ondudi amemwamuru Maalim kulipa shilingi milioni sita kama gharama ya kesi. Duale amepongeza uamuzi huo akisema mahakama imeheshimu uamuzi wa wananchi. Kwengineko mahakama imetupolia mbali kesi ya kupinga kuchaguliwa kwa mbunge wa Bonchari Oroo Oyoika iliyowasilishwa na aliyekuwa mbunge Zebedeo Opore.

Show More

Related Articles