HabariMilele FmSwahili

Wanaotaka kujaza nafasi ya mkurugenzi wa mashtaka ya umma wana leo pekee kuwasilisha maombi yao

Wanaotaka kujaza nafasi ya mkurugenzi wa mashtaka ya umma wana hadi leo saa kumi na moja jioni kuwasilisha maombi yao katika tume ya huduma za umma. Haya ni kwa mujibu wa kamati iliyotwikwa jukumu la kumteua atakayejaza nafais hiyo. Kamait hiyo inayoongozwa na Dkt Elizabeth Muli inasema baad ya kupokea maombi hayo itawakagua wote waliotuma kabla ya kuanza kufanya mahojiano. Iwapo unataka kujaza nafais hiyo, unahitaji kuwa aghalabu tajiriba ya miaka 10 kama jaji au hakimu, shahada ya masuala ya sheria na pia mwenye maadili, mionogni mwa mahitaji mengine. Atakaye fanikiwa atachukau mahala pa aliyekuwa mkuu wa mashtaka Keriako Tobiko baada yake kuteuliwa waziri wa mazingira na rais Uhuru Kenyatta.

Show More

Related Articles