MichezoPilipili FmPilipili FM News

Kombe La Dunia Latua Kenya.

Rais Uhuru Kenyatta siku ya jumatatu alipata heshima ya kulishika kombe la dunia ambalo lilizuru nchini katika ziara ya ulimwenguni kabla ya mashindano yenyewe makuu kuandaliwa nchini Urusi badaaye mwezi Juni mwaka huu.

Rais Kenyatta alijawa na furaha wakati akikabidhiwa kombe hilo lenye uzito wa kilogramu 6.1 na urefu wa sentimita 36 na ambalo linakadiriwa kuwa na thamani ya shilingi bilioni moja fedha za Kenya.

Kombe hilo lilibuniwa kwa mara ya kwanza mnamo mwaka wa 1974 na kampuni kutoka Italia ijulikanayo kama Stabilimento Artistico Bertoni Company na kombe hili hushikwa na marais wa mataifa pamoja na washindi wa kombe hilo pekee.

Hii ni mara ya tatu kwa kikombe cha dunia kuzuru nchini mara ya mwisho ilikua ni miaka ya 2010 na 2013.

Kiongozi wa taifa alitaka ushirikiano na serikali za kaunti ili kukuza talanta za soka kuanzia mashinani na kuhakikisha kama taifa Kenya inatoa timu nzuri ambayo itaweza kufuzu kwa kombe la dunia siku zijazo.

Show More

Related Articles