HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosVideos

Wafanyibiashara wa makaa na changarawe watatiza usafiri,Limuru

Usafiri kwenye barabara kuu ya kutoka Nairobi kuelekea Naivasha ulitatizwa kwa takriban saa nne katika eneo la Limuru , baada ya wafanyibiashara wa makaa na changarawe kufunga barabara hiyo , wakitaka gavana wa Kitui Charity Ngilu atiwe mbaroni kwa madai ya kuchochea wenyeji wa kitui kuteketeza lori za makaa wiki tatu zilizopita.

Ilibidi maafisa wa polisi wawatawanye wafanyibiashara hao, huku gavana Ngilu akifika mbele ya tume ya uwiano na maridhiano NCIC, kabla ya kikao cha kumhoji kuahirishwa.

Show More

Related Articles