HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosVideos

Wakili Adrian Njenga ataka Maraga na makamishna 6 waondolewe

Makamishna saba wa tume ya huduma kwa mahakama wakiongozwa na jaji mkuu David Maraga wanakodolewa macho na zimwi la kufurushwa afisini, kupitia ombi la kupendekeza waondolewe afisini ambalo limewasilishwa kwa uongozi wa bunge la kitaifa.

Wakili kwa jina Adrian Kamotho Njenga amependekeza hilo na kudai kuwa makamishna hao hawajawajibikia afisi waliyopokezwa na pia wanadaiwa kukiuka katiba na hasa sehemu ya sita kuhusu maadili na utendakazi wa wanaojukumika kwenye afisi za umma, pamoja na kuwahujumu majaji waliodhihirisha uhuru wao kwenye maamuzi yao.

Show More

Related Articles