HabariMilele FmSwahili

Polisi huko Meru Kusini wapata mtoto wa miezi 4 aliyeibiwa kutoka Kutus Kirinyanga

Polisi huko Meru kusini wamefanikiwa kumpata mtoto wa miezi minne aliyekuwa ameibwa kutoka kanisa la Jesus Winners huko Kutus Kirinyaga. OCPD wa Meru kusini Baraza Saiya anasema wanamzuilia mshukiwa wa miaka 22 kutoka kijiji cha Matinia, wadi ya Mitheru huko Maara baada ya kupatikana na mtoto huyo. Mamake mtoto huyo Fidelis Mugo anasme alikuwa amemwachia rafikiye mtoto huyo lakini aliporejea bada ya shughuli za kanisa mmoja wa washiirka alikwu ametoweka naye.

Show More

Related Articles