HabariMilele FmSwahili

Mkenya mmoja ataka jaji mkuu Maraga na makamishna 6 wa JSC kutimuliwa

Mkenya mmoja amewasilisha ombi kaitika bunge la taifa akitaka kutimuliwa jaji mkuu David Maraga, naibu wake Philomena Mwilu na maafisa wengine 5 kutoka tume ya huduma za mahakama JSC. Wakili Adrian Kamotho Njenga anasema wawili hawa sawa na Jaji Mohamed Warsame, jaji Aggrey Muchelule, Tom Ojienda, Emily Ominde na Mercy Deche wamekiuka katiba na hasa sura ya sita, kutoweza kufanya majukumu yao kikamilifu na kukosa kufuata sheria katika utendakazi.anawatuhumu kwa kuwadhalilisha baadhi ya majaji na pia kupuuzilia mbali malalamishi yaliyowasilishwa katika tume hiyo dhidi ya baadhi ya majaji.

Show More

Related Articles