HabariPilipili FmPilipili FM News

Wakaazi Wa Kwale Waiomba Serikali Kuwatatulia Tatizo La Uhaba Wa Maji

Huku takriban wakenya milioni 3.4 wakitajwa kuwa hatarini ya kuathirika na kiangazi humu nchini, wakazi wa kilifi mojawapo ya kaunti iliyoko kwenye hatari ya kuathirika na ukame wanaiomba serikali kufanya hima kushughulikia tatizo la maji kufuatia changamoto wanazopitia wakitafuta bidhaa hiyo adimu.

Kulingana na wengi wao kutoka eneo la Bamba vyanzo vya maji ambavyo wamekuwa wakitegemea vimeanza kukauka hali ambayo inawatia hofu endapo makali ya ukame yataongezeka.

Aidha wameitaka idara ya maji katika kaunti hiyo kushughulikia kwa udharura mabomba ya maji yaliyo na kasoro ikizingatiwa kwa sasa wamekosamaji kwa mda wa miezi niwili.

Show More

Related Articles