HabariPilipili FmPilipili FM News

Wasichana Wanyimwa Nafasi Yakujiunga Na Vikosi Vya Usalama Kisauni

Wanawake hawatapata nafasi ya kujiunga na kikosi cha jeshi la KDF mwaka huu eneo la kisauni hapa mombasa, hii ni kulingana na afisa mkuu mwandamizi wa zoezi hilo Willy Lang’at.

Akizungumza wakati wa kuanza rasmi zoezi hilo huko kisauni Lang’at amesema wakaazi wamejitokeza kwa wingi kushiriki zoezi  hilo, hata ingawa ni wanaume watatu pekee watakaosajiliwa kati ya wote watakaohitimu.

Baadhi ya wanawake tuliozungumza nao wameeleza kuhuzunishwa na hatua iliyochukuliwa na wasimamizi wa zoezi hilo kwa kuwanyima nafasi ya kushiriki.

Show More

Related Articles