HabariMilele FmSwahili

Gavana wa Kitui Charity Ngilu ahojiwa na NCIC kuhusu tuhuma za uchochezi

Gavana wa Kitui Charity Ngilu amehojiwa na maafisa wa tume ya uuiano na utangamano NCIC kuhusiana na tuhuma za uchochezi dhidi yake. Ngilu amekuwa akikabiliwa na madai ya kuchochea wakazi wa kaunti yake kuteketeza malori ya kusafirisha makaa kaunti yake kinyume na sheria. Kinara wa Wiper Kalonzo Musyoka aliyeandamana na gavana Ngilu amemtetea dhidi ya madai hayo akidai matamshi yake yalilenga kuzuia uharibifu wa mazingira. pia Kalonzo amedai uchunguzi dhidi ya Ngilu unatishia kuzua uhasama baina ya jamii mbali mbali zinazoishi kaunti ya Kitui.

Show More

Related Articles