HabariMilele FmSwahili

Eugene Wamalwa :Serikali haitoruhusu mkenya yeyeote kufa njaa

Serikali haitoruhusu mkenya yeyeote kufa njaa. Waziri wa ugatuzi Eugene Wamalwa amedokeza kuwa serikali imetenga msaada wa vyakula vitakavyokabidhiwa wakazi wa kaunti mbili za Pwani zilizoathirika na ukame akihutubu kwenye kongamano la kamati ya seneti kuhusu ugatuzi huko Mombasa wamalwa anasema wizara yake itasambaza vyakula TanaRiver kesho kabla ya kuzuru kaunti zingine eneo hilo na kote nchini. Aidha amezitaka serikali za kaunti kuunga mkono marufuku ya serikali ya ukataji miti na kuhimiza upanzi wa miti nchini ili kukabili ukame.

Show More

Related Articles