HabariMilele FmSwahili

Mahakama yahalalisha ushindi wa mbunge wa Starehe Charles Kanyi (Jaguar)

Mahakama kuu ya Nairobi imehalalisha ushindi wa mbunge wa Starehe Charles Kanyi maarufu Jaguar. Jaji Fred Ochieng ameamua kuwa mlalamishi Steve Mbogo hakudhibitisha kuwa uchaguzi ulikumbwa na udanganyifu. Mbogo ametozwa shilingi milion 10 kama gharama ya kesi. Mahakama kuu ya siaya wakati wowote sasa inatarajiwa kutoa uamuzi kuhusiana na kesi ya kupinga kuchaguliwa mbunge wa Gem Elisha Odhiambo. Kesi hiyo iliwasilishwa na aliyekuwa mbunge Jakoyo Midiwo.

Show More

Related Articles