HabariPilipili FmPilipili FM News

Kutoka Fuo Za Pwani Hadi Fuo Za Lake Victoria

Shirika la ndenge la silver Stone sasa limezindua  safari za ndenge kuanzia Mombasa hadi Kisumu

Akizungumza na wanahabari kwenye uwanja wa ndenge wa Moi kaunti ya mombasa, mkurungenzi wa shirika la ndege kaunti ya mombasa Walter Angong amesema abiria watakao safari kuanzia kaunti ya Mombasa kuelekea kaunti ya Kisumu sasa watakuwa na afueni ya usafiri.

Aidha mkurungenzi wa mauzo katika shirika hilo la silver stone Patric Okech amesema kiwango cha malipo ya usafiri kuanzia Mombasa hadi Kisumu ni shilingi elfu kumi huku ndenge hiyo ikitumia dakika 90 kwa safari hiyo.

Hata hivyo Okech amesema wanafuraha kuanzisha usafiri huo ambao utasaidia kuunganisha kaunti hizo mbili kwa upande wa  biashara na shuhguli nyenginezo.

Show More

Related Articles