HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosVideos

Kalonzo atofautiana na Joho kwenye mkutano wa ODM

Juhudi za kuleta kwa pamoja muungano wa NASA kungonga mwamba zilijitokeza peupe hii leo, kwenye mkutano wa viongozi wa kitaifa wa chama cha ODM, baada ya kinara wa NASA Kalonzo Musyoka na gavana wa Mombasa Hassan Joho kuonekana kutofautiana hadharani.
Joho alisistiza chama ni ODM na Kalonzo Musyoka kukashifu viongozi ambao wamekuwa wakizomea uongozi wa chama cha Wiper.
Hata hivyo, kinara wa NASA Raila Odinga alishikilia kuwa NASA iko imara na pamoja licha ya viongozi hao wawili kutofautiana pakubwa huku Musalia Mudavadi akisalia kimya kuhusu haya.

Show More

Related Articles