HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosVideos

Serikali yatangaza Wakenya milioni 3.4 wanahitaji msaada

Huku serikali ikijizatiti kukabiliana na baa la njaa nchini ambapo kwa sasa limewaathiri wakenya millioni 3.4, hali mbaya ya kiangazi inaendelea kukumba kaunti ya Isiolo ambayo imetajwa kati ya nne zilizoathirika pakubwa.
Hali hii imepelekea wagonjwa wanaoishi na virusi vya ugonjwa wa ukimwi kukosa kumeza dawa za kupunguza makali kutokana na ukosefu wa maji na chakula.
Hayo yanajiri huku washika dau katika sekta ya kukabiliana na majanga wakiongozwa na waziri wa ugatuzi Eugene Wamalwa, pamoja na shirika la Msalaba Mwekundu wakifanya kikao cha dharura ili kutafuta suluhu ya kudumu.

Show More

Related Articles