HabariMilele FmSwahili

Matiang’i atoa hakikisho kudumishwa usalama mlima Elgon

Waziri wa usalama wa ndani dr Fred Matiangi ametoa hakikisho la kudumishwa usalama kote nchini kufuatia kuzuka uvamizi ambao umepelekea maafa baadhi ya maeneo nchini. Akizungumza baada ya kuzuru eneo la mlima Elgon kulikozuka mshambuli yaliyopelekea maafa, Matiangi anasema maafisa wake wako radhi kukabiliana na yeyote aliyena nia ya kutatiza usalama wa wananchi. Anasema idara ya polisi imeimarishwa kudumisha usalama amedokeza kuanzia mwezi Agosti mtaala wa polisi utafanyia mabadiliko hasaa kitengo cha kuwasajili makurutu na kwamba waliofuzu taaluma mbali mbali watapewa kipau mbele kwa minajili ya kuleta maarifa yao kuimarisha kikosi hicho

Show More

Related Articles