HabariPilipili FmPilipili FM News

Mohamed Ali Apata Afueni Mahakamani

Mbunge wa Nyali Mohammed Ali amepata afueni baada ya mahakama kuu hapa mjini Mombasa kuidhinisha ushindi wake.

Akisoma hukumu hiyo, jaji wa mahakama hiyo Lydia Achode amesema mlalamishi ambaye ni Said Abdalla hakuwasilisha ushahidi wa kutosha kupinga ushindi huo.

Said Abdalla wa ODM ambaye alikuwa mpinzani mkuu wa MOHAMMED Ali katika uchaguzi wa agosti nane, ameamuriwa kulipa shilingi milioni saba kama gharama ya kesi hiyo.

Baada ya uamuzi huo wafuasi wa Said ABDALLA maarufu Saidoo walianza kuzua vurugu kukabiliana na wale wa Mohammed Ali hatua iliyowalazimu maafisa wa usalama kuingilia kati.

 

Show More

Related Articles