HabariMilele FmSwahili

Rais ampendekeza Nyachae kuhudumu kama jaji wa mahakama ya Africa Mashariki

Rais Uhuru Kenyatta amempendekeza aliyekua mwenyekiti wa tume iliokua ya utekelezaji katiba (CIC) Charles Nyachae kuhudumu kama jaji wa mahakama ya Afrika Mashariki. Nyachae ambaye ni wakili na mwanasiasa sasa anaeleka mjini Dar Salaam nchini Tanzania ambapo mahakama hiyo ina makao yake. Uteuzi wake unajiri miezi miwili tangu jaribio lake kuteuliwa kama mbunge wa bunge la Afrika Mashariki kufeli. Anatarajiwa kuapishwa baadaye leo kwa wadhfa huo mpya.

Show More

Related Articles