People Daily

Shirika La Msalaba Mwekundu Laomba Msaada

Shirika la msalaba mwekundu nchini sasa linawaomba wahisani kusaidia kuchangisha takriban shilingi bilioni moja, zitakazotumika kukabiliana na ukame na uhaba wa chakula unaotarajiwa kulikumba taifa hivi karibuni.

Katibu mkuu wa shirika hilo Abass Gulet amesema pesa hizo zitasaidia pakubwa kukabiliana na makali ya njaa ikiwemo kununua chakula, kusambaza maji, ununuzi wa mifugo miongoni mwa mengine.

Kati ya kaunti zilizotajwa kuwa hatarini ya kuathirika na ukame ni kaunti ya Marasabit, Garissa, Wajir, Kitui, Taita Taveta, Tana River, Kilifi Na Kajiado ,huku mabadiliko ya hali ya anga yakidaiwa kuchangia hali hiyo.

Show More

Related Articles