HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosVideos

Wakenya watolewa wito kuchangisha shilingi bilioni 1 kukabili ukame

Shirika la msalaba mwekundu sasa linawaomba wahisani kusaidia kuchangisha angalau shilingi bilioni moja, zitakazotumika kukabiliana na ukame na baa la njaa unaotarajiwa kulikumba taifa hivi karibuni.
Katibu mkuu wa shirika hilo Abass Gulet amesema kwamba pesa hizo zitasaidia sana kukabiliana na makali ya njaa ikiwemo kununua chakula, usambazi wa maji, ununuzi wa mifugo miongoni mwa mahitaji mengine.
Baadhi ya kaunti zinazotazamiwa kuathirika na ukame ni kama vile, Marasabit, Garissa, Wajir, Kitui, Taita Taveta, Tana River, Kilifi Na Kajiado huku mkengeuko wa hali ya anga ukisemakana kuchangia hali hii.

Show More

Related Articles