HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosVideos

Wafanyibiashara walalamikia kubomolewa kwa vibanda vyao na KENHA

Hali ya taharuki ilitanda katika kaunti ya Mombasa baada ya wafanyibiashara waliokuwa wamejenga vibanda nje ya soko la Kongowea kufanya maandamano huku wakilalamikia kubomolewa kwa vibanda vyao na mamlaka inayosimamia barabara kuu nchini [KENHA] .
Wafanyibiashara hao waliojawa na ghathabu walikwamisha usafiri katika eneo la Kongowea kwa kufunga barabara na hata kuwasha moto kwenye barabara inayoelekea kwenye soko kuu ingawaje maafisa wa polisi waliweza kufika na kuwatawanya.

Show More

Related Articles