HabariMilele FmSwahili

Dr Ekuru Aukot azindua baraza lake la mawaziri kivuli “shadow cabinet”

Kinara wa Thirdway Alliance Dr.Ekuru Aukot amezindua baraza lake la mawaziri kivuli(shadow cabinet) analosema litafuatilia utendakazi wa serikali. Akitangaza wakenya 22 watakaohudumu kwenye baraza hilo, Dr.Aukot amewataja wateule kama wakenya walio na tajiriba katika taalum walizoteuliwa na kwamba watahakikisha uwajibikaji wa serikali. Dr. Aukot aliyemaliza wa pili kwenye marudio ya uchaguzi wa urais Oktoba 26 mwaka jana anasema,hatasitakuikosoa serikali iwapo haitawajibikia utendakazi wake.

Show More

Related Articles