MichezoPilipili FmPilipili FM News

FKF Kutangaza Mkufunzi Mpya Wa Harambee Stars Wiki Ijayo.

Shirikisho la soka nchini FKF limeahidi kuubomoa na kuujenga upya uwanja wa kaunti ya Mombasa ambao awali ulikua na utata kuhusiasana na mwanakandarasi aliyepewa kazi ya ujenzi huo.

Akiongea wakati wa ukaguzi wa kiwanja cha kisasa cha Bomu eneo bunge la changamwe kaunti ya Mombasa rais wa shirikisho la soka nchini Nick Mwendwa amesema kiwanja cha kaunti kitajengwa upya katika hadhi ya kisasa

Kuhusiana na mkufunzi wa timu ya taifa ya Hrambee Stars Mwendwa amedokeza kuwa wiki ijayo kutatolewa tangazo la mkufunzi mpya atakaye chukua nafasi ya Paul Put aliyejiuzulu.

Wakati huohuo ameipongeza serikali ya kaunti ya Mombasa kwa ujenzi wa kiwanja cha Bomu akisema kitatumika kwa mechi ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 20 kati ya harambee stars na timu ya misri mwezi machi

Aidha amesema kutachaguliwa shule malumu amabyo itakua inakuza talanta kutoka kaunti ya Mombasa

 

 

Show More

Related Articles