HabariMilele FmSwahili

Mahakama ya Kitale yaridhia ushindi wa mbunge wa Sirisia John Waluke

Mbunge wa Sirisia John Waluke amepata afueni baada ya mahakama kuu ya Kitale kuridhia ushindi wake katika uchaguzi mkuu wa Agosti Nane. Jaji Anthony Murima ameamua kuwa mlalamishi Levi Malaki hakutoa ushahidi wa kutosha kudhibitisha madai kuwa waluke aliwahonga wapiga kura. Makali pia ameagizwa kulipa gharama ya kesi ya shilingi milino 6. Uamuzi huo umepokelewa kwa shangwe na vifijo miongozi mwa wafuasu wa Waluke.

Show More

Related Articles