HabariPilipili FmPilipili FM News

Wanafunzi Walalamikia Kinyesi Cha Ngombe Shuleni

Wanafunzi wa shule ya msingi ya Kilole  huko Msambweni  Kwale wanalalamikia kukerwa  na kinyesi cha mifugo ambao mara nyingi hufanya sehemu ya  shule hiyo  kama makaazi yao kutokana  na ukosefu  wa ua shuleni humo.

Suleiman Mwabarau mwalimu mkuu  wa shule hio aliyekuwa akizungumza katika halfa  ya kutolewa  kwa visodo kwa wanafunzi wa kike shuleni humo,  amesema kwamba wanatumia muda mwingi kusafisha shule kutokana kinyesi cha ngombe ambacho huwakimejaa shuleni humo.

Mwabarau akiongeza kwamba  wezi wadogo wadogo pia hufanya shule hiyo kama mkaazi yao kutoka na ukosefu wa ua na  kuitaka serikali na wahisani kujitokeza  na kuwajengea ua

Show More

Related Articles