HabariPilipili FmPilipili FM News

Makatibu Na Mabalozi Walioteuliwa Wahojiwa Bungeni

Kamati ya uteuzi bungeni inawahoji makatibu wa kudumu katika wizara walioteuliwa na rais Uhuru Kenyatta pamoja na walioteuliwa kuwa mabalozi.

Akihojiwa na kamati hiyo,aliyekuwa waziri wa mazingira Judy Wakuhungu ambaye ameteuliwa kuwa balozi wa Ufaransa, amehakikisha ataendeleza kazi yake kwa mujibu wa katiba, bila ya kuwa na fikra kwamba kuondolewa katika wadhfa wa waziri hadi Ubalozi ni kumshusha hadhi.

Naye aliyekuwa mshirikishi wa serikali kanda ya  Pwani Nelson Marwa amefika mbele ya kamati hiyo kuhojiwa baada ya kuteuliwa kuwa katibu katika wizara ya ugatuzi.

Akijitetea Marwa amesema kufuatia uzoefu alianao katika sekta ya usalama atahakikisha ugatuzi unatekelezwa kikamilifu.

Show More

Related Articles