HabariMilele FmSwahili

Mamia ya wafanyikazi wa nyumbani waandamana jijini Nairobi

Mamia ya wafanyikazi wa nyumbani wameandamana kulalamikia kile wanakitaja kama kutelekezwa pasi na kutambuliwa kama wafanyikazi wengine nchini. Waandamanaji hao wamepiga kambi nje ya makao ya bunge wakitaka kilio chao kisikizwe na bunge ambapo wanataka kusajiliwa kama wanachama wa hazina ya NSSF na bima ya NHIF. Wakipokelewa na wabunge Omboko Milemba na Godfrey Osotsi, wamelalama kwamba wametengwa kwa muda na wakati umefika wao kutambuliwa. Wabunge hao wamehaidi kuwasilisha lalama zao bungeni.

Show More

Related Articles