HabariMilele FmSwahili

Gullet : Wakenya milioni 3.4 wameathirika na baa la njaa nchini

Wakenya milioni 3.4 wameathirika na baa la njaa nchini. Katibu wa shirika la msalaba mwekundu Abbas Gullet anasema hali hiyo inatokana na kiangazi cha muda mrefu ambacho kinashuhudiwa nchini. Akiongea baada ya kumtembelea gavana wa Nyeri Mutahi Kahiga, Gullet amesema kaunti za Isiolo, Kilifi, Kajiado, Wajir na  Tana River ndizo zilizoathirika zaidi na zinahitaji msaada wa dharura. Gullet anasema shirika hilo litazindua ombi rasmi siku ya Alhamisi wiki hii kwa wakenya, wahisani kutoka nchi za nje na wafadhili kuwasaidia waathiriwa. Aidha amezitaka serikali za kaunti kushirikiana na serikali kuu kutafuta suluhu la kukabiliana na janga hilo.

Show More

Related Articles