HabariPilipili FmPilipili FM News

Kaunti Kamishna Kaunti Ya Kwale Anyooshewa Kidole Cha Lawama

Wakulima kaunti ya Kwale wamemtaka waziri wa ardhi Farida Karoney kuingilia kati mzozo wa ardhi ya diani Settelment Scheme baada ya kudai kuwa ardhi hiyo imevamiwa na polisi jana usiku na kujaribu kuondoa vigingi walivyoweka ikiwemo kubomoa nyumba zao.

Wakulima hao wamemshutumu kamishna wa kaunti ya Kwale kwa kutumiwa vibaya na mabwenye ili kunyakua ardhi yao ambayo wamekuwa wakiishi kwa zaidi ya miaka 20.

Wakulima hao wamewataka wafanyikazi wa serikali kuhakikisha wanatekeleza haki kwa wenyeji, kwani hatua ya kuwavunjia nyumbao zao kwenye shamba hilo huenda ikawafanya kuchukua sheria mikononi mwao

Show More

Related Articles