HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosVideos

Walimu wasio wenyeji katika kaunti ya Wajir sasa wanataka uhamisho

Walimu ambao sio wenyeji wa kaunti ya Wajir lakini wanafunza huko , wameihimiza tume ya kuwaajiri walimu nchini tsc kuwapa uhamisho mara moja, wakisema kuwa hawatasubiri kuuawa na wanamgambo wa Al shabaab.
Walimu hao ambao walifanya mkutano hii leo na TSC , walisema kuwa serikali imezidi kunyamaa huku wanamgambo wa Al shabaab , sasa wakiwavamia hadi shuleni mwao.
Uamuzi huo umeonekana kuwiana na ule ulitolewa na chama cha walimu wa shule za upili KUPPET kikitaka walimu hao kuhamishwa.

Show More

Related Articles

Check Also

Close