HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosVideos

Waziri Keriako Tobiko aonya dhidi ya uharibifu wowote wa mazingira

Waziri wa mazingira Keriako Tobiko ameonya vikali wale watakaopatikana na kosa la ukataji miti kiholela au kuhusika uharibifu wowote wa mazingira.
Tobiko aaliyeingia afisini kwa mara ya kwanza leo amewataka maafisa wa mamlaka ya mazingira nchini NEMA kuendeleza juhudi zao za kuwanasa wanaokaidi marufuku iliyowekwa dhidi ya matumizi ya mifuko ya plastiki.

Huku hayo yakijiri waziri wa ardhi Farida Koroney ambaye pia ameanza kazi rasmi hii leo ameapa kupambana na wanyakuzi wa ardhi na kusawazisha shughuli katika wizara hiyo.
Lenox Sengre alihudhuria hafla hiyo na kutuandalia taarifa hii.

Show More

Related Articles