HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosVideos

Watu wanne wauawa na watu wanaoaminika kuwa wanachama wa SLDF

Hofu imetanda katika eneo la mlima elgon kufuatia mauaji ya watu wanne katika kijiji cha Sarai usiku wa kuamkia leo na watu wanaoaminika kuwa wanachama wa kundi lililopigwa marufuku la Sabaot Land Defense Forces SLDF.
Mwili wa mmoja wa waliouawa ulipatikana bila kichwa huku ikiaminika kuwa wahalifu hao waliondoka nacho.
Wakati wa shambulizi hilo ng’ombe kadhaa walipigwa risasi na kukatwa katwa kwa mapanga.

Show More

Related Articles