HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosVideos

Wazazi wataka kuongezwa muda kupata vyeti huku makataa yakitimia kesho

Huku siku ya mwisho ya kuwasilisha vyeti vya kuzaliwa vya wanafunzi haswa wa shule za chekechea na za msingi ikiwa ni hapo kesho, hii leo wazazi wengi walikuwa katika harakati za kuzipokea kutoka kwa vituo mbalimbali nchini.
Hii ni ili wanafunzi hao wapate kusajiliwa katika mfumo wa kuwatambua unaofahamika kama Nemis, na kama mwanahabari wetu Grace Kuria anavyotueleza, iwapo kufikia kesho kama mzazi hutakuwa umewasilisha cheti hicho, bado itambidi mwanao asajiliwe mwaka ujao, na hii inamaanisha atarudia darasa ambalo yuko sasa.

Show More

Related Articles