MichezoPilipili FmPilipili FM News

Paul Put Ajiuzulu Kama Mkufunzi Wa Harambee Stars

Mkufunzi mkuu wa timu ya taifa harambee stars paul put amejiuzulu rasmi kama mkufunzi wa timu ya taifa.

Put amejiuzulu akisema sababu binafsi ndizo zimemfanya aweke kikomo mkataba wake na shirikisho la soka humu nchini.

Kujiuzulu kwa mbelgiji huyu kunajiri mwezi mmoja kabla ya kipute cha kufuzu kwa kombe la bara afrika mwezi machi dhidi ya Ghana

Also read:   Waki weru wa iharo gwikururia

Shirikisho la soka FKF limethibitisha kujiuzulu kwa mkufunzi huyo kwa masikitiko huku ikidaiwa huenda akawa anaelekea kuwa mkufunzi wa timu ya taifa ya Guinea

Na hali hiyo imetajwa kama kurudisha nyuma mipangilio ya kufuzu kwa kombe la bara afrika mwaka ujao.

Stanley Okumbi atashikilia ukufunzi mpaka pale mkufunzi wa kudumu atapatikana.

Also read:   Harambee Stars kuchuana na Iraq kwenye mechi ya kirafiki leo

Put aliweka mikataba novemba mwaka jana mkataba wa miaka miwili lakini sasa amesema tosha kwa kuikufunzi timu ya Kenya.

Itakumbukwa Put aliisaidia Kenya kushinda kombe la Cecafa Senior Challenge dhidi ya Zanzibar

 

Show More

Related Articles

Close

Adblock Detected

Please consider supporting us by disabling your ad blocker